Monday, July 14, 2014

WATU WAWILI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA KUFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI KILIMANJARO




Breaking Nyuzzzz: WATU WAWILI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA KUFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI KILIMANJARO
Zaidi ya watu wawili wanadhaniwa kupoteza maisha baada ya kufunikwa na kifusi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa miamba kwa ajili ya uchongaji wa tofari. Tayari mpaka sasa mwili wa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Bless Adrian, mkazi wa kijiji cha Nganjoni wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro. Juhudi za kutafuta miili mingine inaendelea licha ya kukabiliwa na changamoto ya zana za kufukulia kifusi.