Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi. Monica Mwamunyange akibadilishana kadi na Profesa Liu Xueyi kutoka Chuo kikuu cha Southwest Jiatong, wakati mkufunzi huyo na wanafunzi wa chuo hicho walipotembelea wizara ya Uchukuzi leo mchana kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya reli hasa reli ya mwendo kasi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange, akifafanua jambo kwa Wakufunzi na wanafunzi wanaochukua shahada za Uzamili na Uzamivu katika Reli kutoka Chuo Kikuu cha Southwest Jiatong, wakati walipotembelea Wizarani hapo kujifunza na kubadilishana uzoefu hasa kwenye usafiri wa Reli, leo mchana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bi Monica Mwamunyange (wa nne kutoka kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi, wanafunzi na sehemu ya wakurugenzi wa Wizara ya Uchukuzi, wakati wanafunzi hao wanaochukua shahada za uzamili na uzamivu katika Eneo la Reli kutoka chuo kikuu cha Southewest Jiatong walipotembelea Wizarani hapo leo mchana ili kubadilishana uzoefu hasa katika treni za mwendo kasi. Aidha chuo hicho kimeahidi kubadilishana uzoefu na Chuo che Reli Tabora ili kujenga uwezo katika masuala ya Reli. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi)