Sunday, July 06, 2014

SONGOMA ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUWACHANGANIA DAWA WATEJA WAKE




SONGOMA ACHEZEA KICHAPO BAADA YA KUWACHANGANIA DAWA WATEJA WAKE
Hii nimetumiwa na mdau wangu jana usiku:
Nimeshuhudia leo jioni hii mganga huyo akipokea kichapo toka kwa wateja wake,hao wateja wake ambaye ni mtu na mkewe walikuwa wakilalamika kwamba walikuja kwa mganga huyo kwa lengo la kupatiwa dawa kwa ajiri ya mume kuongeza nguvu za kiume,lakini tangu aanze kutumia dawa hiyo ndio kwanza benteke hana uwezo kabisa hata wa kutoa pasi.
Mke alidai kwamba dawa aliyopewa mumewe imemfanya benteke anyong'onyee kabisa hasa anapokutana na timu pinzani.baada ya maelezo hayo mganga alidai kuchanganya dawa kwani aliyowapa ilikuwa ni ya kumpunguzia nguvu benteke na si ya kumuongezea nguvu.aliwapa dawa nyingine aliyodai kwamba benteke sasa atakuwa na nguvu balaa ya kufunga magoli .baada ya kupewa dawa hiyo wameondoka wote mume na mke wakiwa na furaha ,cha kushangaza mke ndiye aliyeonekana kuwa na furaha zaidi kuliko mwathirika mwenyewe ambaye ni mume.