Thursday, July 10, 2014

JK KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA



JK KATIKA ZIARA YA KIKAZI MKOANI TANGA
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Pikipiki mmoja wa maafisa watendaji kata Wilaya ya Kilindi Bi.Elizabeth Mwita muda mfupi kabla ya Rais Kuhutubia Mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi. Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi kombe katibu wa TFF Wilaya ya Kilindi Bwana Omari Javu wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Songe Kilindi jana.Kombe hilo lijulikanalo kama Kikwete cup litashindaniwa katika ligi ya wilaya ambapo mshindi atakabidhiwa kombe hilo na zawadi nyinginezo kibao
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi Mkoani Tanga 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara mjini Songe Kilindi mkoani Tanga. Picha na Freddy Maro wa Ikulu