Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizindua ununuzi wa karafuu kwa msimu wa mwaka 2014-2015 katika kituo cha ZSTC Mkoani Pemba,(kushoto) Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui ,zoezi hilo lilifanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiangalia zao la karafuu alipotembelea katika shamba la Bw.Said Sinani (hayupo pichani) Shumbageni Kusini Pemba akiwa katika ziara maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Bw.Said Sinani (kulia) baada ya kulitembelea shamaba lake la mikarafuu leo akiwa katika ziara Mkoa wa Kusini Pemba. Picha na Ramadhan Othman.