Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba akikanusha vikali taarifa za aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa na kueleza kuwa mtu huyo alipatiwa notice ya kuondoka nchi ambapo Juni 10 mwaka huu aliamriwa kuondoka nchi Juni 13 huku akisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa Kia kama ilivyoelezwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice ya kuamriwa kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo ulizingatia taratibu zote za kisheria.
Nanomba alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika kusini na alikua mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita na kuwaonya. Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi na hivyo kuwataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchi vinginevyo watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano.
Kwa kipindi cha Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.
Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
Pia wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini.
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)