Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Dubai, UAE, unapenda kuwatangazia Umma wa Watanzania kuwa Kampuni na Wakala wa Ajira ya CAREER FARAH LEISURES ya UAE, imetangaza kazi zifuatazo kwa watu wenye sifa zinazohitajika kuziomba.
Hivyo basi, Ubalozi Mdogo unawaomba Watanzania wenye sifa za kazi zilizotangazwa, kuziomba mara moja na kuwasilisha maombi hayo kama ilivyoonyeshwa kwenye tangazo hapo juu. Aidha, ili kurahisisha ufuatiliaji wa maombi yenu, tunakuombeni mtume pia nakala ya maombi yenu kwa anuani ya barua pepe ya Ubalozi Mdogo kama ifuatavyo:
Attention: Mheshimiwa Balozi Mdogo,
Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dubai, UAE.
Ubalozi Mdogo unapenda kuwafahamisha kuwa, tangazo hili litatolewa pia kwenye Gazeti la Serikali la DAILY NEWS.
Akhsanteni, na tunawatakia kila la kheri waombaji wote.