Wednesday, June 04, 2014

SPIKA EALA BADO NGANGARI WABUNGE WAANZA KUJITOA


SPIKA EALA BADO NGANGARI WABUNGE WAANZA KUJITOA
Margaret-Zziwa-the-Speaker-of-the-East-Africa-AssemblyMahmoud Ahmad Arusha
WABUNGE wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) wamesisitiza kuwa hatua ya kumgo'oa Spika wa Bunge hilo Magraret Zziwa ziko pale
pale licha ya wabunge wa Tanzania watatu kutoa saini zao juu ya msimamo huo.Aidha wabunge wa Tanzania wakiongozwa na Shyrose Bhanji walipoeleza kuwa  wameondoa saini zao kwenye azimio la kuunga mkoo kuon'olewa kwa
spika huyo.Wabunge hao walianza hoja hiyo mara baada ya Zziwa  kumaliza kusoma sala  na kukaribisha kusomwa kwa bajeti lakini haikufanyika kwaniwabunge walianza kupiga makelele kulalamika kuwa hakuna ajenda ya kuong'olewa kwa spika kwenye shughuli za siku.Hapo ndipo Bhanji aliposimama na kusema kuwa  wabunge wa Tanzania Adam Kimbisa, Shyrose Bhanji na Mariamu wameondoa saini zao katika

azimio la kuunga kung'olewa kwa Spika Zziwa madarakani.
Alisema ni kweli Zziwa  anamapungufu  yake lakini mchakato wa kumuondoa madarakani una hatua zake moja baada ya nyingine lakini pia wakati wakiwa njiani sasa nimegundua kuna ajenda ya siri ambayo imezidi yale mapungufu ya Spika na ndio lengo la kutaka kumuondoa madarakani.
Alisema  amejaribu kuelewesha kwamba kama wabunge hao wanataka kwenda na jambo hili si mbaya wakienda nalo hatua kwa hatua ila kwa hapa baadhi ya wabunge hawataki wanataka jambo hili lichukuliwe bila utaratibu.
Alisema bunge hilo ilikuwa wanatakiwa kusoma Bajeti ya Afrika Mashariki tangu juzi lakini mpaka sasa hivi wabunge wamekataa katukatu wanataka suala la kung'olew a spika ndio lipewe kipaumbele.
Alisema wabunge wa Tanzania walikuwa wamesaini na kuamua kutoa saini zao  na walijiuliza  mara mbili je kuna ajenda nyingine iliyoongezeka ya kutaka kumuondoa spika, wakasema kwamba sisi tunaishia hapo na hatutaendelea na mchakato huo.
Na utaratibu wa kumuondoa Spika unasema lazima kuwe na saini za wabunge wanne kutoka kila nchi wanachama na kwasababu Tanzania saini zimebakia 2 basi kwa sasa azimio hili limeshakufa halina nguvu tena kisheria.
Lakini pia wananchi wa  (EAC) wamekuwa wakijiuliza tumekuja kufanya nini kwenye hili bunge, badala yake wanatuona kama viongozi tulikuja kuangalia ajenda zetu binafsi badala ya maslahi ya wananchi wa jumuiya.
"Nimeliangalia suala hili kwa mapana yake na kuona masuala ya wananchi wa afrika mashariki ndio jambo muhimu linalopaswa kupewa kipaumblele na si ajenda hii ambayo pengine kuna ajenda iliyojificha nyuma yake".
MWINYI AGOMA KUTOA SAINI YAKE
Spika anatuhuma zinazomkabili kutoka kwa wabunge na mpaka hivi sasa hatutajua kama tuhuma hizo ni za kweli au si za kweli.
Kwa hiyo ni vyema hizo tuhuma zikapelekwa kwenye Kamati husika zifanyiwe uchunguzi ili Kamati inayohusika ya Sheria ikaangalie itafute ushahidi halafu itoe maelezo mbele ya bunge ili bunge lifanye maamuzi
Sasa inawezekana tuhuma zikawa ni sahihi lakini pia inawezekana tuhuma zikawa si sahihi sasa kukipatikana ushahidi kamili na kuna uzito sasa hapo Bunge ndio litaamua atoke ama asitoke
Mimi  ndio maana sijaondoa saini yangu kwenye azimio la kumng'oa Spika kwasababu naelewa kwamba kuna tuhuma, na hizi tuhuma ziende kufanyiwa uchunguzi na ndio maana sijatoa saini yangu, hizi ni tuhuma na sisemi kama huyu mama kafanya au hajafanya mimi sijui ukinuliza kafanya nini
sijui lakini zipo tuhuma sasa kwanini zisifanyiwe kazi??? Zikifanyiwa kazi hapo tutajua kama kweli kakosea au hajakosea.
Anasisitiza kuwa  hawawezi kuondoa saini zao sasa hivi badala yake wanapaswa waache azimio hilo liendeleee hadi mwisho ili hatua ya kutoa ushahidi itakapofika basi wao ndio watakuwa na nafasi ya kujitoa kwamba hawamo wala hawaungi mkono jambo hilo.
Lakini pia hoja nyingine inakuja kwamba kama mtu ameonyesha kutoka moyoni hana nia ya kusaini ili kumuondoa madarakani Spika kwanini unamlazimisha  mambo hayo ndio yamesababisha msuguamo wa kisheria baina ya wabunge.
Lakini kiutaratibu kama jambo limeshaingia ndani ya Bunge huwezi kuingiza jambo jingine wakati lile la kwanza halijamalizwa hapa kuna hoja mbili Bajeti inatakiwa kuletwa bungeni lakini je wanaweza kuileta wakati hili la kumng'oa Spika halijamalizwa? Kimsingi ni suala la kisheria na wanasheria wanasema lazima limalizwe kwanza
Naye Mwanasheria wa EAC na Bunge hilo ,Wilbrt Kahwa alisema,kutolewa kwa saini za wabunge watatu wa Tanzania haina maana kwasababu saini hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kuunga mkono jambo hilo katika hatua za awali kwa ajili ya kutengeneza azimio, sasa azimio tayari limeshatengenezwa  na lipo ndani ya Bunge.
Na azimio likishafika huko kuna taratibu zake za kuindoa huko bado hatujafikia hatua hiyo  na si hatua hii ya kuondoa saini ambazo kazi yake ilikuwa ni ya awali mwanzo huko tumeshatoka.
Saini hizo 3 haziwezi kuzuia azimio la kumngoa Spika kwani tayari ilishafika bungeni azimio linaenda mbele halirudi nyuma.
Awali wabunge hao kutoka nchi za EAC walikuwa na malalamiko ya kutokuwa na imani na Zziwa na kuazimia kumn'goa lakini kadri siku zinavyokwenda baadhi ya wabunge wanarudi nyuma na kujitoa katika msimamo huo na kutaka  kuachan na hoja hiyo ili bajeti ya EAC  iweze kupitishwa