Wednesday, June 18, 2014

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOADHIMISHWA WILAYANI MKURANGA



SIKU YA MTOTO WA AFRIKA ILIVYOADHIMISHWA WILAYANI MKURANGA
Mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid akifuatilia sherehe hizo katika viwanja vya Shule ya Msingi Kiparang'ada. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Kiparang'anda Mhe Karu Amani Karavina, na Kulia ni Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima.
Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akizungumza machache wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika,yaliyofanyika Juni 16 katika shule ya msingi Kiparang'anda,wilayani Mkuranga.Kushoto ni Mgeni Rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid
Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akikabidhi Sare na Vifaa vya shule kwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kiparang'anda,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku Mtoto wa Afrika.
Picha ya Pamoja baada ya kukabidhiana vifaa mbali mbali.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mhe Juma Abeid  akijaribu kusukuma Baiskeli ya walemavu iliyotolewa na Mke wa Mbunge wa Mkuranga ajili ya watoto wenye uhitaji wa vifaa hivyo.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Mkuranga Sharifa Nabalanganya akisoma risala ya Wilaya kwa Mgeni Rasmi.
Afande Hamis, Msemaji wa dawati la Jinsia akiwaelezea Wazazi na Watoto kuwa huru kuripoti unyanyasaji wowote unaofanywa kwa Watoto.
Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mkuranga akielezea Haki na wajibu wa Watoto.
Mdau Faidha Salum akifurahia jambo wakati wa Sherehe za Mtoto wa Afrika.
Wadau wa Haki za watoto wakifuatilia sherehe hizo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kiparang'anda wakisoma shairi Juu ya Watoto kulindwa ili wasome kwa amani na furaha.
 Sehemu ya Wanafunzi wa shule hiyo.

Mke wa Mbunge wa Mkuranga,Mama Naima Malima akigawa zawadia kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Kiparang'ada wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika,yaliyofanyika Juni 16 katika shule hiyo,wilayani Mkuranga.