Tuesday, June 17, 2014

Shoti ya Umeme yasababisha Kukosekana Umeme Baadhi ya Maeneo Zanzibar leo



Shoti ya Umeme yasababisha Kukosekana Umeme Baadhi ya Maeneo Zanzibar leo
                     Hii ndio breaker liyoungua na kusabibisha maeneo ya mjini Ubguja kukosa umeme leo

 Mafundi kutoka ZECO wakiwa katika harakati za kutengeneza panel iliyoleta hitilafu za umeme na kupelekea maeneo yote ya mji wa Unguja kukosa umeme

Baada ya kukamilika kwa matengenezo

Kuamkia alfajiri ya leo ya tarehe 17/06/2014 maeneo yate ya mji wa Unguja na maeneo jirani ya mji wa Unguja yalikumbwa na ukosefu wa umeme uliotokea kuanzia majira ya saa 11 asubuhi hadi saa 7 mchana kulikosababishwa na hitilafu zilizotokea katika moja ya panel zake na kuungua kwa breaker katika kituo cha kusambazia umeme Mtoni mjini Unguja.
Katika kipindi hicho chote njia (laini)  za maeneo ya mji wa Unguja zinazopokea umeme wa  mkondo wa 11kV yalikosa umeme.  Njia (laini) hizo ni njia ya Mtoni-Mpendae, Cotex, Saateni 5 na Saateni 6.
Miongoni mwa maeneo yaliyokosa umeme ni:
Laini ya Saateni 5: Saateni, Mkele, Muungano, Jang'ombe, Mpendae, Kidongochekundu, Kilimani, Kikwajuni.
Laini ya Saateni 6: Mlandege, Darajani, Malindi, Kiponda, Forodhani, Mkunazini, Gongoni, Mwembetanga, Shangani, Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Laini ya Cotex: Mwembemakumbi, Kwaalamsha, Kariakoo, Mwembeshauri, Misufini, Maruhubi, Mabanda ya Ng'ombe, Mtoni, Beit el Ras, Kibweni, Bububu, Mwanyanya, Dole, Kizimbani, Kinumoshi.
Laini ya Mtoni-Mpendae: Chumbuni, Makadara, Darajabovu, Kilimahewa, Sebleni, Nyerere, Magogoni, Magomeni, Mwanakwerekwe, Melinne Uzi, Kijitoupele, Kwarara, Nyarugusu, Fuoni, Chunga, Welezo, Kinuni, Masingini, Kianga, Meli sita, Mwera, Koani, Kidimni, Dunga, Mgenihaji, Uzini, Bambi, Pagali.
Tahadhari kwa wateja ni kwamba wakati wowote ule umeme unapozimika ni vyema kuzima vifaa vya umeme vilivyowazi ili kuepuka athari ya kuunguza vifaa vyao wakati umeme utakaporudi.