Thursday, June 12, 2014

Moto wateketeza soko la mitumba la karume jijini Dar



Breaking Newssss: moto wateketeza soko la mitumba la karume jijini Dar usiku huu
Pichani ni mwanga wa moto unaotoka ndani ya soko la mitumba la Karume lililopo maeneo ya Ilala jirani na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam  ambalo linateketea na moto usiku huu. 
Taarifa zilizotufikia katika meza ya usiku zinasema kuwa moto huo ulianza kidogo kidogo katika baadhi ya vibanda ambavyo wenye navyo walikuwa hawapo, kabla ya kushika  kasi na kuteketeza kila kitu kilichopo kwenye eneo  hilo. Tunafuatilia kujua kama kuna watu walioathirika na moto huo pamoja hasara iliyopatikana na chanzo chake