Nyota wa Ivory Coast Gervinho akishangilia bao lake na Didier Drogba.
MAGOLI mawili ya vichwa ya Wilfried Bony na Gervinho yaliyopishana kwa sekundi 98 yameipa ushindi wa kwanza Ivory Coast kwenye mchezo wa kundi la C wa kombe la dunia na kuilaza Japan mabao 2-1 mjini Recife.
Bony aliifungia Ivory Coast bao la kusawazisha katika dakika ya 64 na Gervinho akaongeza bao la ushindi mnamo dakika ya 66.
Japan walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa nyota wao Keisuke Honda, na baada ya hapo Ivory Coast waliendelea kupoteza nafasi za kufunga.
Kutokana na uzembe huo wa washambuliaji wa Ivory Coast ilionekana ndoto ya kufuzu hatua ya 16 kutoka kundi C inaweza kupotea kutokana na ushindi waliopata Colombia dhidi ya Ugiriki katika kundi lao la C.
Tembo hao kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika walimuacha nahodha wao , Didier Drogba katika kikosi kilichoanza ambapo aliingia katika dakika ya 62 akichukua nafasi ya Die na alifanya vizuri kwa dakika hizo alizocheza.
Gervinho na Wilfried Bony walifunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na kuwapa ushindi Ivory Coast.
Kikosi cha Ivory Coast: Barry, Aurier, Bamba, Zokora, Boka (Djakpa 75), Tiote, Yaya Toure, Die (Drogba 62), Gervinho, Bony (Konan 77), Kalou.
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Gbohouo, Viera, Kolo Toure, Bolly, Akpa Akpro, Diomande, Gradel, Sio, Sayouba.
Waliooneshwa kadi ya njano: Bamba, Zokora.
Wafungaji wa Magoli: Bony 64, Gervinho 66.
Japan: Kawashima, Uchida, Morishige, Yoshida, Nagatomo, Yamaguchi, Hasebe (Endo 53), Okazaki, Honda, Kagawa (Kakitani 86), Osako (Okubo 68).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Nishikawa, Gotoku Sakai, Kiyotake, Aoyama, Konno, Inoha, Saito, Hiroki Sakai, Gonda.
Waliooneshwa kadi za njano: Yoshida, Morishige.
Mfungaji wa bao: Honda 16.
Idadi ya watazamaji: 40,000
Mwamuzi: Enrique Osses (Chile)

Hata hivyo kuingia kwa Drogba kuliwafanya Japan waanze kumfikiria yeye tu, wakati huo huo Bony na Gervinho waliweza kumalizia krosi mbili kutoka kwa beki wa kulia Serge Aurier ambaye ameripotiwa kuwindwa na Asernal baada ya kumpoteza Bacary Sagna aliyejiunga na Manchester City wiki hii.
Licha ya kufunga mabao 65 katika mechi 101 alizoichezea nchi yake, mshambuliaji huyo mkongwe alianzia benchi na kumuacha kijana Bony ambaye anamzidi miaka 11 aanze na alionesha kuwa alikuwa chaguo sahihi.
Twende kazi: Bony akishangilia na mchezaji mwenzake didier Drogba baada ya kuufanya ubao wa matangazo usomeke 1-1.
Keisuke Honda akiifungia Japan bao la kuongoza
Honda alinyoosha msuli si mchezo