Mkazi
wa kitongoji cha Budushi, Kata Mwendakulima, wilaya ya Kahama mkoani
Shinyanga Antony Joseph 25- 26 amefariki dunia mchana wa leo baada ya
kujitupia kwenye kisima cha maji akiwakimbia askari wa Jeshi la Polisi .
Mwenyekiti
wa kitongoji cha Budushi Zainab Kazi amesema Tukio hlo limetokea mchana
wa leo baada ya Joseph kukamatwa kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia
ya utapeli, kwenye mtego ulioandaliwa eneo la benki ya NMB mjini
Kahama.
Kazi
amesema, Kijana huyo alituhumiwa kuwatapeli vijana wa kijiji cha
Lugunga mkoani Geita ambao walifika katika kituo cha polisi Kahama kutoa
taarifa ndipo mtego ulipoandaliwa na kufanikiwa kukamatwa.
Amesema
Joseph aliwadanganya vijana hao kwamba ni mfanyakazi wa Benki ya Nmb
kahama ambapo aliwaambia wampe hela ili awasaidie kuwafungulia Akaunti
na kuwatafutia kazi mjini humo.
Kufuatia
utapeli huo vijana hao waliweka mtego kwa kumpigia Simu kwa lengo la
kumpa fedha zingine ndipo alipokamatwa na kuamriwa kwenda kwake ili
kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake.
Baada
ya kuwa amefikishwa nyumbani kwake Mwendakulima akiwa chini ya ulinzi
alimtishia kumpiga askari ndipo alipopata mwanya wa kukimbia na
kujitupia kisimani.
Juhudi
za kumwokoa zilifanyika ambapo walimtupia kamba ili atoke huku naye
akikataa kutumia kamba hiyo kujiokoa hadi alipopoteza maisha kabla ya
Kikosi cha zima Moto kufika eneo hilo na kumwopoa akiwa amefariki.