Na Sultani Kipingo
Kamati ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 ilikuwa na nyota watano wa zamani wa Brazil (pichani wakiwa na maafisa wa chama cha soka cha Brazil) waliowahi kuwika katika michuano hiyo tokea mwaka 1958 ilipofanyika nchini Sweden. Kamati hiyo, iliyoundwa January 2013 inaundwa na wachezaji wakongwe kina kutoka kushoto juu:
Amarildo Tavares da Silva (wa tatu toka kulia) , José Roberto Gama de Oliveira (Bebeto), Carlos Alberto Torres, Marta Vieira da Silva, Ronaldo Luis Nazario de Lima (wa pili kulia) na Mário Jorge Lobo Zagallo (kushoto).
Watano kati ya wanakamati hao ambao wamepewa Ubalozi wa FIFA waliwahi kuchezea Brazil wakati nchi hiyo ilipofanikiwa kunyakuwa kombe hilo la dunia. Nao ni Mário Zagallo (mwaka 1958 nchini Sweden), Amarildo (waka 1962 nchini Chile), Carlos Alberto (mwaka 1970 nchini Mexico), Bebeto (waka 1994 nchini Marekani), na Ronaldo (mwaka 2002 nchini Korea ya kusini na Japan).
Balozi mwingine ni mwanamama Marta Vieira da Silva ambaye ni mshindi mara 5 wa tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa wanawake katika miaka ya 2006, 2007, 2008, 2009 and 2010.
Ronaldo alisema baada ya kuteuliwa: "Ni muhimu tukawa makini maana mbele yetu tuna kazi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa viwanja, kuchagua mahali ambapo timu ya Taifa itapiga kambi na viwanja mahususi vya mazoezi, na pia kufikia maamuzi muhimu ya kihistoria kama vile kuzindua kauli mbiu ya michuano na Mwanasesera wa Kombe la Dunia la FIFA."