Kaimu Mkurugenzi Dr. Samwel Lazaro, Meya wa Jiji la Mbeya Atanus Kapunga, Mkandarasi Nadhra Iqbal Singh wa kampuni ya Nadhra Engineering &Construction company Limited,Naibu Meya Chieforder Fungo, Mkandarasi Mshauri
Liberate Materu akiongea
soko Jipya
Hawa ni Madiwani , Wakuu wa Idara na wataalam
Meya wa Jiji Atanus Kapunga akiongea
Mkandarasi
Mkurugenzi akiongea
Naibu Meya akiwa na Mkandarasi
Meya akiwa na Mkandarasi
Waandishi wa Habari
ziara
BAADA ya kusuasua kwa muda mrefu kukamilika kwa ujenzi wa Soko la Kimataifa la Mwanjelwa jijini Mbeya,kulikotokana na Mkandarasi aliyekuwa akijenga kushindwa kukamilisha kutokana na muda aliyopewa na kujitoa, Soko hilo limepata Mkandarasi mpya.
Umaliziaji wa jengo la soko hilo unatarajiwa kuanza Julai Mosi mwaka huu baada ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kushinda kesi dhidi ya mkandarasi wa awali kutoka Kampuni ya Tanzania Building Works ya jijini Dar es Salaam.
Makabidhiano ya mradi huo kwa mkandarasi mpya kutoka Kampuni ya Nandhra Engineering & Construction Company(MD) na Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, yalifanyika hivi karibuni katika majengo hayo yaliyopo Mwanjelwa jijini hapa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kapunga alisema hatua ya Halmashauri kumkabidhi soko hilo mkandarasi huyo mpya ni baada ya yule wa awali kushindwa kukamilisha ujenzi wa soko kwa wakati.
Alisema Julai 2012 soko hilo lilipaswa kukamilika na kukabidhiwa kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya jambo ambalo halikufanyika licha ya kupewa muda wa ziada kwa awamu tatu za wiki 20 ambapo tena alishindwa kukamilisha hadi Julai 19, mwaka 2013 alipoandika barua ya kuvunja mkataba.
Alisema kutokana na changamoto hizo ujenzi wa soko hilo ulisimama kwa zaidi ya miezi 10 tangu Mkandarasi wa awali asitishe mkataba wake na kwamba ujenzi huo unatarajia kuanza Julai Mosi mwaka huu na kukabidhi soko hilo Marchi 2015.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Dk. Samwel Lazaro, alisema mkandarasi huyo anatarajia kutumia shilingi bilioni 5.0 katika kukamilisha ujenzi wa soko hilo ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 80 na kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 11 kati ya Bilioni 13 .
Alisema katika kiasi hicho cha fedha cha shilingi bilioni 13 kiasi kilichobakia ni shilingi Bilioni 1.8 hivyo kuilazimu Halmashauri hiyo kukopa tena kiasi cha fedha cha shilingi Bilioni 3.5 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo.
Kwa upande wake, Mkandarasi mpya Nadhra Singh alihidi kuwa atahakikisha kazi hiyo itakamilika katika kipindi walichoandikiana kwenye mkataba hivyo serikali kuondoa mashaka.
January 25,2010 serikali ilimpa miezi 18 mkandarasi kutoka Kampuni ya Tanzania Bulding Works Limited ya jijini Dar es Salaam kuhakikisha soko hilo linakamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya Agosti 24/ 2012 lakini alishindwa kwenda na muda wa makubaliano hivyo kusababisha kuvunja mkataba na halmashauri.
Ujenzi wa Soko hilo ni kutokana na kuteketea kwa moto kwa soko la awali mwaka 2006 na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya 2000 walionguliwa maduka yao.
Na Mbeya yetu