Huo msalaba uuonao hapo ni taa za magazri zilizo katika foleni mishale ya saa moja jioni kwenye makutano ya barabara za Morogoro road na Nelson Mandela jijini Dar es salaam. Hakika kuna haja ya kutafuta njia mbadala za kupunguza foleni ya magari katika jiji hili. Ushauri wa bure kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Boresheni njia za pembeni ili magari yaweze kupungua katika barabara hizi kuu.
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii