Tuesday, June 17, 2014

Balozi Seif akagua shughuli za uwekezaji na hifadhi ya mazingira katika visiwa vya Bawe na Changuu



Balozi Seif akagua shughuli za uwekezaji na hifadhi ya mazingira katika visiwa vya Bawe na Changuu
Msimamizi wa mradi wa uhifadhi wa Makobe katika kisiwa cha Changuu Nd.Suleiman Mnemo akitoa maelezo ya uhifadhi wa viumbe hao adimu duniani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyetembelea kisiwa cha Changuu.
Balozi Seif akikagua baadhi ya majengo ya Hoteli zilizomo ndani ya kisiwa cha Changuu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uwekezaji katika sekta ya Utalii . Kulia ya Balozi ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Leisure Hoteli inayoendesha mradi wa hoteli Bawe na Changuu Bwana Freddy Tenga na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk.
Balozi Seif akikagua moja ya vyumba mardadi vilivyopo katika majengo ya Hoteli ya Leisure iliyopo Kisiwa cha Changuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Kushoto akiwa pamoja na Waziri wa anayesimamia Utalii Mh. Said Ali Mbarouk wakiangalia mazingira ya kuvutia ndani ya eneo la Kisiwa cha Changuu.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Leisure Hoteli na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali aliyofuatana nao wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii katika Visiwa vya Bawe na Changuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara maalum ya kukitembelea Kisiwa cha Bawe kilichopo Magharibi ya Mji wa Zanzibar kuona shughuli za uwekezaji katika sekta ya Utalii. Kulia ya Balozi Seif ni:- Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.