Muonekano wa mbele wa basi la NBS T719 AZC baada ya kugonga basi la Princes Muro T892 BUR lililokuwa likitokea Dar
kwenda Mwanza eneo la Kimara.
Basi la Princes Muro T892 BUR likitokea Dar kwenda Mwanza limegongwa nyuma na basi la NBS T719 AZC likiwa safarini kuelekea Tabora eneo la Kimara leo.
CHANZO cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi la Princes Muro aliyekuwa akiendesha basi lenye namba za usajili T892 BUR ambapo akiwa upande wa kulia wa barabara, ghafla alichepuka upande wa kushoto kwa lengo la kumshusha mfanyakazi mwenzake mahala ambapo si kituo cha kushusha abiria.