KOCHA wa Holland, Louis van Gaal amekataa kujibu maswali yaliyomuhisha na kibarua cha ukocha wa Manchester United.
Mdachi huyo anajiandaa kurithi nafasi ya David Moyes Old Trafford lakini bado klabu haijatoa taarifa rasmi.
Van Gaal ambaye pia alihusishwa na Tottenham, kwa sasa yuko na kikosi chake cha timu ya taifa ya Holland akikiandaa kwa michuano ya Kombe la Dunia ambapo katika mkutano wake na waandishi wa habari kuelekea kutajwa kwa wachezaji watakaokwenda Brazil, hakuwa katika hali ya kuzungumzia hatma yake.
"Hapana, sitasema chochote kuhusu hilo. Niko hapa na kikosi cha Holland. Sio kama kocha wa Manchester United," alisema pale alipoulizwa kuhusu safari ya Old Trafford.
"Mnapaswa kusubiri hadi kila kitu kitakapokamilika au pelekeni maswali hayo kwa Manchester United au pengine klabu nyingi yoyote ile.
"Sitaongea neno lolote kuhusu hilo."