Monday, May 19, 2014

Henry Kilewo:Sheikh Ponda Katibu wa UAMSHO Aachiliwe Huru na Mashtaka Yake Yote Yafutwe

 
 
 
 
Henry Kilewo Amefunguka Kuhusu Sheikh Ponda kwenye Ukurasa wake wa Facebook , Soma Hapa chini alichosema:

"Kama William Lukuvi,Janeth Mbene na Martha (Mkuu wa Wilaya ya Kiteto) bado wapo madarakani kuitumikia serikali inayojitangaza kulinda amani ya nchi basi Sheikh Ponda katibu wa UAMSHO aachiliwe huru na Mashtaka yake yote yafutwe.
Haiwezekani wabaguzi na wachochezi wa siasa za Udini na Ukabila kama hawa wawe madarakani achilia mbali kuwa huru huku Sheikh Issa Ponda akikandamizwa na kufunguliwa mashtaka ya uchochezi
Lukuvi alituhumiwa kufanya uchochezi Kanisani na kisha Bungeni hali kadhalika Janeth Mbene.Hawa nao ni Mawaziri.Anayefanya uchochezi Msikitini,kanisani au Hekaluni na kuhatarisha amani ya nchi kwa maslahi ya kisiasa na ya kidini wote wapimiwe kipimo kimoja bila kujali vyeo au hadhi.Tuwe wapenda haki.Tusiogope kusema ukweli.
Serikali imefanya uchochezi kwa kuwaacha watu hawa Huru huku Sheikh Issa Ponda akinyimwa uhuru.Taifa la Double Standard,Serikali inayopalilia unafiki kwa kuendekeza na kuchochea Chuki Miongoni mwa jamii.Hatuwezi kujenga umoja na kusonga mbele kwa tabia hizi na matendo haya yenye sura mbaya isiyotakiwa katika karne hii ya watu waliostaarabika
The Double Standard Policies of the claimants of Human Rights,Freedom of Worship,Freedom of Expression are further becoming exposed every passing day.
Ni jambo la ajabu kuwa kuna vijana wa CCM wametumika kwenda kumsanifu mama Maria Nyerere na kumlisha maneno ili kuficha aibu ya kauli za kibaguzi za akina Lukuvi
Mama Maria Nyerere aliwaambia ukweli kuwa watawala hawasikilizi wananchi na kisha kuonya kuwa Taifa litaingia kwenye machafuko
Alinukuliwa akilalamika pia kuwa kuna watu wanamchagulia hadi magazeti ya Kusoma? Jamani hiki si kinyume kabisa cha Tangazo la Kimataifa la Haki za Binadamu na kinyume kabisa na Sheria za nchi ambazo zimetungwa kwa mujibu wa Katiba ambayo imetoa haki ya kupata habari na pia uhuru wa maoni? Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanyagwa hadi kwa Mjane wa Baba wa Taifa?
Kikundi cha vijana wanaojiita wazalendo wa Chama cha Mapinduzi kilitumwa kwenda kumtumia Mama Maria kwa maslahi ya chama chao na baadhi ya kambi za Urais ndani ya chama
Ni jambo la ajabu vijana hao kutangaza kuwa watazunguka nchi nzima kueleza kuwa Mwalimu Nyerere ametukanwa.
Hawa ni vijana wasaliti kwa taifa na wanafiki wasiojua wanataka nini ndani ya nchi yao
Hawakumbuki historia kuwa kijana Mwenzao Sethi Benjamini alifariki akiwa safarini kwa matembezi ya kuunga mkono Azimio la Arusha lililojenga misingi ya utaifa na kujenga uadilifu kupitia miiko ya uongozi lakini yale aliyoyafia Sethi Benjamini ,yamepuuzwa na kutupiliwa mbali na watawala wenye nia ovu na taifa hili kisha vijana hawa wasaliti wa Sethi Benjamini na Mwalimu Nyerere wanakubali kutumika kuufunika uchafu huu.
Mwalimu Nyerere katika Hotuba zake amekua akikemea ubaguzi wa kidini na kikabila .Lukuvi na wenzake kuendelea kushikilia nyadhifa za serikali ni matusi makubwa kwa Mwalimu Nyerere na pia ni Kejeli kufanya ziara Nyumbani Kwa Mama Maria kabla ya Kushinikiza chama na serikali yao kuwachukulia hatua wabaguzi hawa na pia kufanya shinikizo la kisera ndani ya chama chao kurudia misingi ya Azimio la Arusha ambayo ilikua Kikwazo kwa Mafisadi" Hernry Kilewo