Mhe. Balozi Naimi Aziz (wa tatu kulia) akiongoza tukio la kuwasha tochi kama ishara ya mafanikio na utekelezaji wa Masharti ya Baraza hilo katika kuleta ufumbuzi wa migogoro barani Afrika. Kushoto kwa Mhe. Naimi Aziz ni Mhe. Erastos Mwencha, Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na kulia ni Balozi Smail Chergui, Kamishna wa Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika.
Mhe. Naimia Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Afrika, akitoa hutuba ya ufunguzu katika Mjadala wa Wazi (Open Session) wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mwaka 2004. Katika mjadala mada mbali mbali ziliwasilishwa na kujadiliwa ikiwemo mafanakio, changamoto na namna ya kuhakisha kwamba bara la Afrika linamaliza migogoro inayoendelea ifikapo 2020 ( Silencing the guns by 2020).
Bw. Samwel Shelukindo, Afisa wa Ubalozi akishiriki katika mjadala huo ambao ulikuwa chini ya uwenyekiti wa Mhe. Balozi Naimi Aziz, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwa mwezi Mei 2014.
Baadhi ya wajumbe wakishiriki katika mjadala huo wa wazi wa kuazimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo.