Profesa Ibrahim Lipumba akikaribishwa na Mchungaji Peter Msigwa (mbunge wa Iringa Mjini )kuhutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza
Huu ndio ulikuwa muitikio wao, wakisisitiza serikali tatu kama walivyotoa maoni yao kwa Tume ya Katiba |
Mchungaji Msigwa akiamsha hali kwa wananchi hao |
Profesa Lipumba akionesha rasimu iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kujadiliwa na bunge maalumu la katiba |
Danda Juu wa NCCR-Mageuzi alikuwepo pia na akazungumza machache anayofahamu kuhusu rasimu hiyo, msisitizo ukiwa ni serikali tatu kama ilivyopendekezwa na katika rasimu |
Diwani wa kata ya mivinjeni Iringa Mjini, Frank Nyalusi alikuwepo na akarusha lawama kwa jeshi la Polisi kwa kutisha watu ili wasipate katiba wanayotaka |
Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Allein alikuwa mshehereshaji wa mkutano huo wa Ukawa |
Moja ya mabango yaliyopamba mkutano huo na ujumbe wake kama unavyosomeka |