Pamoja na ujenzi mzuri wa kituo hiki cha abiria wavukao kutoka Sengereama kuelekea Mwanza mjini kwenye Ziwa Victoria, lakini suala la usalama hapa ni ziro kabisa, magari hayo pichani yakisubiria kivuko lakini hakuna kizuizi chochote kinachozuia hata kwa dharura kama ikitokea bahati mbayha gari moja kugonga mwenzake. Lakini hata hivyo hakuna sababu yoyote ya magari haya kusubiri kivuko kwenye eneo hili la karibu na maji wakati eneo la kutosha lipo
Magari yakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye Kivuko cha Mv Misungwi, umbali wa kuvuka kwenye eneo hili nitofauti na ule umbali wa Kigamboni na Posta ambao huchukua dakika tano , hapa ni mwendo wa dakika 20 kufika ng'ambo ya pili.
Tatizo la kuondoa Kivuko kabla ya watu hawajaishi kuingia nalo hujitokeza maeneo mengi ya vivuko sababu haijulikani, pichani kushoto mfanyakazi wa kivuko akiondoa kamba iliyofungiwa kivuko kabla ya watu hawajaisha kuingia na kivuko kimeanza kutoka, nakuwafanya abiria hao kukimbilia kwa kasi huku wengine wakiwa na watoto wadogo.
Mandhari ya majengo ya kumpumzikia abiria ni nzuri na ni bora zaidi ipo haja ya kuendelea kuimarisha utunzaji wake
Kiwango cha Ubebaji wa mizigo ni Cha kutosha kwa kivuko hiki kulingana na idadi ya watu waliopo, hata hivyo kuna vivuko viwili ambavyo hupishana kwa zamu.
Mwonekano wa eneo la Kando ya Ziwa Victoria.
-->