Watu watatu akiwemo mtoto mdogo wameumizwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba kwaa jiwe lililoporomoka kutoka mlimani jijini Mwanza.
Waliokumbwa na ajali hiyo ni Bw. Msalam Husein ambaye ni dereva (30) na mkewe Bi. Nadia Grecian ambaye ni mama wa nyumbani (25) pamoja na kichanga wao Asfati Mslam (aliyechini ya umri wa mwaka).
Tukio hilo limetokea leo hii majira ya saa 6:00 mchana katika nyumba wanayoishi kilima cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani B Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja na kwamba ni majira ya mchana watu hao mke na mume walikuwa wamejipumzisha kitandani, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali hiyo.
Mtoto Asfati Mslam alifariki dunia jana majira ya saa 9 na dakika kadhaa za alasiri katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure alikokimbizwa yeye na wazazi wake mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia mawe yaliyoporomoka kutoka kwenye msingi wa nyumba iliyo eneo la juu mlimani jijini Mwanza. Mtoto Asfati Mslam amezikwa kwenye makaburi ya Waislamu ya Ngara Kirumba eneo la Mlimani B.
Nyumba ambayo kuta zake zilibomolewa na mawe ya msingi wa nyumba iliyo juu yake.
Msingi wa nyumba iliyo eneo la kimo cha juu toka nyumba iliyovunjwa ukuta na kutokea ajali.
Picha na G.Sengo