Wanahabari, Jenfrida Hongoa na Abby Nkungu kutoka klabu ya SINGPRESS, wakisikiliza kwa makini mafunzo
Waandishi wa habari, washiriki wa mafunzo ya siku moja juu ya vita dhidi ya ukatili wa watoto wa kike na wanawake mkoani Singida
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka asasi isiyo ya kiserikali mjini Singida-SIAC, Bw. Hudson Kazonta akitoa mafunzo kwa wanahabari
Singida
Oktoba 08,2012.
WANAHABARI wameelezwa wana mchango mkubwa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike, kwa kuandika taarifa sahihi zinazohusiana na madhara yatokanayo na ukatili nchini.
Mwezeshaji wa mafuzo hayo, Hudson Kazonta, kutoka asasi siyo ya kiserikali mkoani Singida inayojulikana kwa jina la SIAC, alisema hayo kwenye mafunzo ya siku moja juu ya vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto na wanawake.
Kazonta alisema zaidi ya watoto 4,000 walifanyiwa vitendo vya ukatili mwaka jana mkoani Mara, na kuongeza kuwa kuna njia nyingi za unyanyasaji zinazofanyika ndani ya jamii na kusababisha madhara makubwa kwa walengwa, ikiwemo kuathirika kiakili.
Alisema ukatili unaozungumzwa, hufanywa sana na watu wakubwa kuliko watoto, nahivyo kuleta madhara makubwa katika jamii siku za usoni.
Naye katibu wa asasi ya SIAC, Cecilia Munishi, inayojihusisha na elimu ya kutokomeza mila zenye madhara mabaya kwa wanawake na watoto wa kike,kama vile ukeketaji, ndoa za utotoni, ubakaji na kurithi wajane, alisema mkoani Singida kuna watoto wanaokeketwa.
Alisema baadhi ya maeneo mkoani Singida ngariba kwa kushirikiana na wazazi wamebuni njia mbadala ya ukeketaji, ambapo huweza kusugua sehemu za siri kwa vidole, kabla ya kuweka tumbaku na chumvi kwa watoto wadogo wa kike.
Kwa mujibu wa Cecilia, asasi yake imeamua kushirikiana na wanahabari wa Singida, wasaidie kufichua na kuelimisha jamii kuhusianana athari za ukatili.
Na Elisante John