|
Mbunge wa Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya GODFREY ZAMBI akimkaribisha Mkuu wa mkoa ABASI KADORO jimboni kwake kwa ajili ya Ufunguzi wa ofisi ya kisasa ya kata ya Mlangali.
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akivishwa Skafu na skauti wa kata ya Mlangali wilayani Mbozi kabla ya kufungua jengo jipya la ofisi ya kata hiyo. |
|
Mkuu wa wilaya ya Mbozi DKT.MICHAEL Y.KADEGHE akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa ABASI KANDORO kabla ya kufungua jengo hilo
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akifungua Ofisi ya kata ya Mlangali iliyogharim zaidi ya shilingi Milioni 38 |
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akimuonesha Mbunge wa jimbo hilo Madhaifu ya fundi wa jengo hilo, ambapo alisikitishwa na kitendo cha Mlango wa Mninga kupakwa rangi ikiwa ni pamoja na mbao za mlango huo kutobanwa vizuri hali inayopelekea kuwepo kwa matobo mlangoni |
|
Mkuu wa mkoa ABASI KANDORO akimtaka fundi wa jengo hilo kutoa sababu ya kupaka rangi mbao za mininga ikiwa ni pamoja na kupaka ripu dirisha, hata hivyo alimtaka fundi kuhakikisha ripu hiyo inaondolewa kwenye ubao na kuhakikisha ubao unapigwa msasa ili kuonesha uhalisia wa mbao iliyopo. |
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akipanda Mti mbele ya ofisi hizo kwa lengo la kuhamsisha jamii utunzaji wa mazingira. |
|
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mbozi na Momba LEVISON CHILEWA akipanda naye mt Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dkt.MICHAEL Y.KADEGHE akipanda mt |
|
Mbunge wa Mbozi Mashariki na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya GODFREY ZAMBI akipanda mti mbele ya ofisi za kata ya Mlangal
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akicheza ngoma ya kinyakyusa baada wachezaji wa ngoma hiyo ambao wengi wao ni wazee wakicheza kwa ustadi hali iliyomlazimu kunyenyuka kwenye kiti na kwenda kujiunga nao
|
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akabidhiwa uchifu Mbozi,huku machifu hao wakitoa onyo kwa mtu atakaye jaribu kupuza maagizo ya chifu huyo mpya ndani ya Mbozi na mkoa kwa ujumla |
|
Mkuu wa mkoa wa Mbeya ABASI KANDORO akihutubia maelfu ya watu wa tarafa ya Iyula ambao walihudhuria ufunguzi wa ofisi ya kata ya Mlangali. Katika Hotuba yake Kandoro alisistiza Umoja na mshikamo, utii wa sheria bila shuruti, ushirikiano katika kuendeleza na kukuza shughuli za kimaendeleo, pembejeo za kilimo ambapo aliwataka wakulima kutokubali kurubuniwa na mawakala wadanganyifu kwa kurubuniwa kupewa pesa badala ya mbolea. Hata hivyo amesema kuwa Ruzuku itatolewa kwa mbolea ya Minjingu na sio vinginevyo. Kuhusu mabaraza ya kata Kandoro ataka faini isizidi elfu 10 na kuwepo kwa haki bila upendeleo huku rufaa ya watu kwenda mahakamani zitolewe kwa haki.
|
Habari kwa hisani ya Bwille Media Mbeya