Rais wa Shirikisho la Ngumi, Taifa (BFT), Alhaji Shaban Mintanga (pichani kati) ameachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kukutwa hana kesi ya kujibu.
Mintanga alifikishwa Katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya Julai 2008 hata hivyo aliendelea kusota ndani hadi leo alipoachiwa na mahakama hiyo.
jaji Twaib kumuachia huru mshitakiwa kwa kifungu cha sheria namba 293 (1) ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Ilikuwa ni furaha isiyo kifani kwa ndugu na jamaa za mshitakiwa huyo baada ya ndugu yao kusota rumande muda mrefu sasa yu huru.
Jaji Dk Fauz Twaib alisema kuwa anamuachia huru kwasababu kati ya mashitaka mawili yaliyokuwa yakimkabili, kula njama na kusafirisha dawa za kulevya, hakuna lililothibitishwa kutendwa na mshitakiwa.
Hakuna uthibitisho kuwa mshitakiwa alikula njama kwasababu haikutolewa ushahidi kuwa mshitakiwa ni wapi na wakati gani alitenda kosa hilo.
Aidha jaji huyo alisema pia kuwa haikuthibitishwa mshitakiwa alisafirisha dawa hizo kwasababu yeye hakusafiri na pia washitakiwa waliokamatwa huko nchini Mauritius walimtaja mtu anayeitwa Mika kuwa ndiye aliyewapa na kuwamezesha katika hoteli iliyoko Manzese hapa jijini.
Jaji Fauz alisema kuwa kama ni kuhusishwa na mashitaka hayo basi ilikuwa ni Mika ambaye upande wa mashitaka ulidai kuwa bado unamtafuta.
Upande wa jamuhuri ulikuwa na mashahidi wane tu baada ya Jaji huyo kuwalazimisha kufunga ushahidi, toka mwanzoni mwa mwaka huu kesi hiyo ilikuwa ikiahirishwa tu kutokana na upande wa mashitaka kushindwa kuleta mashahidi wengine mahakamani katika wakidai kuwa mashahidi hao muhimu wako Mauritius ambao ni wafungwa waliokamatwa na dawa hizo hivyo inafanyika utaratibu wa kuwasafirisha.
Mintanga alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kula njama na kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa Kilo 4.8, kutoka Tanzania kwenda Mauritius kwa kuwatumia wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa pamoja na watu waliosafiri katika msafara huo ambao walidaiwa kuwa ni mashabiki.
Jaji huyo alisema kwa mujibu wa ushahidi ushahidi uliotolewa ni dhaifu hakuna ushahidi unaoonesha Mintanga alikula njama na alisafirisha dawa za kulevya kama mashitaka yanavyoeleza.
Jaji huyo anaungana na hoja ya wakili wa mshitakiwa, Jerome Msemwa hakuna ushahidi dawa zilizokamatwa kuletwa mahakamani au picha za dawa hizo.
Utata wa uzito wa dawa hizo pia ushahidi wa upande wa mashitaka ulikadiria uzito na thamani za dawa hizo kwa kupiga simu bila kuziona.
Aidha ni ngumu kwasababu dawa hizo zilikamatwa nchini Mauritius hakuna ushahidi wa dawa hizo na kesi hiyo ambayo inamkabili mshitakiwa Mintanga, ushahidi wa Charles Ulaya ambaye ni mpelelezi wa shauri alidai uzito wa dawa hizo ulikuwa Kg 4.8 na ushahidi mwingine unaonesha ni Kg 6.
|