![]() |
Kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa na Salim Abri Asas akifungua mkutano huo leo katika ukumbi wa jumba la maendeleo Kitanzini mjini Iringa |
![]() |
wajumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoa wa Iringa |
Picha ya chini ni .Wagombea wa nafasi ya uenyekiti UVCCM mkoa wa Iringa kutoka kushoto mwanahabari wa Nuru FM Abba Ngilangwa , Mwalimu wa sekondari ya Mwembetogwa Ramadhani Baraza na Mwanahabari wa gazeti la Mwananchi Tumaini Msowoya wakiwa ukumbini leo

![]() |
Mwanahabari Tumaini Msowoya anayegombea kiti mkoa wa Iringa |
Kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Salim Abri Asas ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa wa Iringa amewataka vijana wa CCM mkoa wa Iringa kujiajiri wenyewe katika sekta zisizo rasimi kama njia ya kujikwamua katika maisha.
Amsema hayo leo wakati akitoa salam zake kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Orofea mjini Iringa .
Asas amesema kuwa moja kati shughuli ambazo zinaweza kuwakwamua vijana hao katika dimbwi la umasikini ni pamoja na kufanya kazi kwa juhudi zaidi na kuwa na shughuli zao wenyewe za uzalishaji mali.
Hivyo amesema kuwa ili chama cha mapinduzi CCM kiweze kuendelea kuwa mfano kwa vyama vingine vya siasa ni lazima vijana wa CCM kuwa mafano kwa vijana wa vyama vingine ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa juhudi zaidi badala ya kushinda vijiweni katika makundi ambayo hayana faida katika Taifa.