Mgeni rasmi Dk. Mary Mwanjelwa akizindua jarida la shule.
Mkuu wa Shule hiyo, Dk. Binamungu Mukasa akitoa hotuba yake
Mgeni rasmi katika mahali hayo, Dk. Mary Mwanjelwa akitoa hotuba yake
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti mmoja wa wanafunzi waliofanya vizuri, David Michael Machuche wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti, Asinta John Mpesa wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa akimkadhi cheti mwalimu wa shule hiyo, Sista Anastella wakati wa mahafali ya 14 ya Shule ya Sekondari ya Loyola yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
David Michael Machuche (katikati) akiwa na wahitimu wenzake
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Loyola wakiingia kwenye ukumbi wa mahafali shuleni hapo Mabibo jijini Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Loyola wakimsikiliza mgeni rasmi wa mahafali ya 14 shuleni hapo.
Baadhi ya wawakilishi wa Chuo cha St. Paul cha London Uingereza wakisikiliza hotuba ya mgeni rasm, Dk. Mary Mwanjelwa (MP)
NA SALUM MKANDEMBA
UONGOZI wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Dar es Salaam, umeshauriwa kuandaa programu maalum ya kuwasomesha wahitimu wa kidato cha nne katika kipindi cha kusubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano.
Ushauri huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mary Mwanjelwa, katika mahafali ya 14 ya kidato cha nne shuleni hapo ambako alikuwa mgeni rasmi.
Mwanjelwa alisema ili kuwajengea wahitimu hao mazingira ya utayari wa masomo ya kidato cha tano, kuna haja ya shule kuandaa ratiba itakayowapa wanafunzi masomo hayo, ili kutopoteza maarifa waliyoyapata shuleni hapo.
Pamoja na hilo, mbunge huyo aliupongeza uongozi wa Loyola kwa kuifanya kuwa moja ya shule za kupigiwa mfano nchini na kuwataka walimu kuhakikisha wanaendelea kulibakisha juu jina la shule hiyo.
Mwanjelwa akaupongeza uongozi wa shule hiyo chini ya Mkuu wa Shule, Binamungu Mukasa, na kusema akiwa mmoja wa wazazi wa wahitimu hao 182, anatambua kazi kubwa inayofanywa na timu nzima ya walimu shuleni hapo katika kuwajenga vijana kielimu, kiimani na kimaadili.
Katika hotuba yake, Binamungu aliwashukuru wazazi na kusema mafanikio ya kielimu kwa wahitimu hao yametokana na juhudi za pamoja za wao (wazazi), walimu na wanafunzi.