Mbunge mstaafu wa jimbo la Mufindi kusini kupitia CCM Mhe.Benito Malangalila (pichani kulia )amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya wilaya ya Mufindi mjini Mafinga mkoani Iringa ,Malangalila amepata kuwa mbunge wa jimbo hilo toka mwaka 2005 hadi 2010 alipoamua kustaafu na kumwachia mbunge wa Sasa Bw Menderady Kigolla (CCM) hata hivyo mbunge huyo kabla na baada ya kustaafu alikuwa akiugua mara kwa mara na muda wote toka alipoamua kuachana na siasa alikuwa akiugua na kujipumzisha nyumbani kwake. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amina.