Thursday, September 20, 2012

TIGO YAMZAWADIA MSHINDI WA PILI NA WA MWISHO WA ‘TIGO BEATS’.

 

Mkazi wa Kijiji cha Kigugu, Kata ya Sungaji, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, Hamis Athuman Pita (19), ( kushoto ) akipokea hundi ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni kumi, kwa Msimamizi wa Kampuni ya Tigo Kituo cha Morogoro Neema Mashingia, anayehudumia pia na Mikoa ya Dodoma, Iringa, Mbeya na Ruvuma baada ya kijana hiyo kushinda shindano ya promosheni ya Tigo Beats , iliyoendeshwa na Kampuni hiyo kuanzia Mei 21 hadi Julai 19, mwaka huu, ( kati kati) ni Mfanyakazi wa Tigo Morogoro, Vissa Majitaka.

Tigo imetoa  zawadi kwa mshindi wa pili na wa mwisho  wa droo ya 'Tigo Beats.' Hamisi Athumani kutoka Turiani Morogoro ndiye mshindi wa shilingi 10,000,000/= aliyepatikana wiki iliyopita katika  bahati nasibu  iliyofanyika kwa mfumo wa kompyuta chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu. 

"Tunajitahidi kutoa huduma bora ambazo tunataka ziboreshe maisha ya wateja wetu," alisema Alice Maro, Afisa uhusiano wa Tigo. "Kwa sababu  ya maendeleo  ya kiteknolojia, tunataka kuwa  pamoja katika maisha ya wateja wetu kila siku na kuwa sehemu ya mafanikio yao," alisema.

Tangu tarehe 21 Mei hadi 19 julai 2012,mteja aliye download  nyimbo yoyote mpya ya Tigobeatz  kwa kuchagua namna mbalimbali za kumwezesha mteja kudownload wimbo kama: kubonyeza alama ya  nyota (*) wakati wanapowapigia ndugu, jamaa au rafiki zao,  kwa kutuma  herufi ya wimbo wowote kwenda 15050, au kwa kupiga 15050 na kununua wimbo wanaoupenda anakuwa tayari amejiingiza katika droo hiyo. Wateja watajiongezea nafasi ya kushinda kwa kila wimbo watakaokuwa wana-udownload.

Tigo inapenda kuwakumbusha wateja wake kutumia  huduma mpya ya 'Tigo Islamic Portal,' kwa ajili ya mwezi huu Mtukufu wa  Mfungo wa Ramadhani. Kwa kupiga namba 0901904444 wateja wa Tigo wataweza  kupata neno katika kitabu cha Koran, Dua,' Hadeeth na Qasida, pamoja na ushauri wa kidini kutoka kwa Shehe. Mteja atatozwa shilingi 0.25/= ili kupata huduma hii kwa mara ya kwanza na kutozwa shilingi 15/= kila siku.