Friday, September 21, 2012

TIGO KUWEKEZA KWA WAJASIRIAMALI KWA MAISHA BORA YA WATOTO TANZANIA.




 Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Mh. Sophia Simba kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Tigo Reach for Change” yenye lengo la kuwekeza kwa wajasiriamali watakaotoa mawazo thabiti yatakayosaidia kuboresha maisha ya watoto.

Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akihutubia wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Mh. Sophia Simba akimpongeza mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez kwa hotuba nzuri aliyoitoa, kulia ni Ofisa wa huduma za jamii wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael akipiga makofi.
Waziri wa Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Mh. Sophia Simba akitoa hotuba wakati wa mkutano huo.
Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo kitengo cha huduma za jamii , Esther Palsgraaf akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Tigo Reach for Change”.
Wadau na waandishi wa Habari wakifuatilia kwa umakini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkurugenzi wa Tigo Tanzania Diego Gutierrez.
Kampuni ya Simu za mikononi ya Tigo kwa kushirikiana na Taasisi ya Sweden inayojulikana kwa jina la Reach for Change leo wamezindua kampeni ya ‘Tigo Reach for Change’ ambayo imelenga  kuwatafuta na kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo wenye mawazo imara yatakayosaidia maisha ya watoto Tanzania.
Njia bora ya kuleta mabadiliko ya kijamii ni kwa kuwapatia zana sahihi watu ambao wako tayari kubuni miradi ambayo itaweza kujiendesha yenyewe kwa mda mrefu”alisema Diego Gutierrez,Meneja mkuu wa Tigo Tanzania,tunaamini katika maendeleo na kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii tunayoihudumia.Tunaamini kila mtoto ana haki ya kuishi maisha kamili na tutawapatia nafasi hiyo katika mradi huu.”aliongeza
Wajasiriamali wenye nia na uwezo wanakaribishwa kuwakilisha mawazo yao kuomba kwa kupitia tovuti ya Tigo au kupeleka mawazo hayo kituo chochote cha huduma kwa wateja cha Tigo. Maombi yote yatapitiwa na jopo la wataalamu na watakaoshinda watajiunga na mpango wa miaka mitatu ambapo mawazo hayo yatabadilishwa na kuwa endelevu kwa kuingia ubia, pia watapata dola za kimarekani 25,000 kila mwaka kwa miaka yote mitatu pamoja na ushauri kutoka wafanyakazi wa ngazi za juu wa Tigo.
Kwa mda ambao mshindi atakuwa akipokea hela kutoka Tigo, mawazo yake yatakuwa yakifanyiwa tathmini ili kuhakikisha kuwa ni bora mpaka hapo mradi utakapoendelezwa na kukamilika.
Kuwajali na kuwapa huduma bora watoto wetu sio jukumu la serikali peke yake”alisema mheshimiwa Sophia Simba waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.”tunawapongeza Tigo kwa mkakati huu ambao hautasaidia tu maisha ya watoto na vijana Tanzania bali pia itajumuisha kufanya kazi na wajasiriamali wadogo ambao wanakaa ndani ya jamii moja na watoto hao hao,hivyo wanaelewa zaidi matatizo yao.”alisema
Wajasiriamali washindi watatu watatangazwa Desemba mwaka huu na mpango huu utaendelea kwa miaka mitatu, kwa kuchaguliwa washindi watatu kila mwaka.
Reach for change ni Shirika la kujitolea lililopo Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik,shirika anzilishi la Tigo, Kampeni ya kutafuta wajasiriamali kwa mkakati wa reach for change ulianzia huko Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia 2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa Ghana Afrika ambayo imeweza kuripoti mafanikio makubwa kwa kusaidia kuinua maisha ya watoto zaidi ya 140,000.
Tigo imeanza rasmi utafutaji wa wajasiriamali katika nchi zinazotoa huduma Africa kwa kuzinduliwa kwanza Rwanda ikifuatiwa na Tanzania, Congo DRC,Senegal na mwisho itakuwa Chad.