Monday, September 24, 2012

Taswira Mbalimbali Katika Tamasha La Fiesta Mjini Iringa



Mmoja wa wasanii chipukizi aliyeibukia kwenye shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,kutoka Mkoani Mbeya aitwaye Ney Lee pichani akionesha kipaji chake cha kuimba jukwaani  kwenye uwanja wa Samora,mkoani Iringa katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Iringa kwenye muonekano mpya wa tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa samora.
Ni mkali mwingine kutoka Morogoro kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa katika uwanja wa samora,kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Ni mkali mwingine kutoka jijini Mwanza kupitia shindano la Serengeti Supa Nyota 2012, Young  KIller akikamua vilivyo mbele ya wakazi wa mji wa Iringa  ndani ya uwanja wa samora,pamoja na muonekano mpya wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012.(picha zote kwa hisani ya  http://issamichuzi.blogspot.com)