Profesa Abdull Shariff, akiwasilisha mada yake kuhusu Wajibu na Dhima ya Vyombo vya habari kuripoti habari za Muungano. katika Mkutano wa (Role of the Media in the Union Debate) ulioandaliwa na Baraza la Habari Tanzania kwa Waandishi wa habari wa Zanzibar.
Mzee Hassan Nassor Moyo akizungumza na Waandishi akisisitiza jambo alipokuwa akiwasilisha mada yake, katika mkutano wa waandishi katika ukumbi wa hoteli ya Mazsons Shangani.
Muasisi wa Muungano waTanzania na Zanzibar Mzee Hassan Nassor Moyo, akitowa Mada yake kuhusu Historia ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika, kwa Waandishi wa habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Hoteli ya Mazsons Shangani, kuhusu Vyombo vya Habari katika Mjadala kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkutano huo umeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania.
Mwakilishi kutoka Jumuiya ya ANGOZA Zanzibar Hassan Khamis akichangia moja ya mada zilizowasilishwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Habari Zanzibar na kuwashirikisha Waandishi wa Habari Vyama vya Siasa na Taasisi binafsi Zanzibar.
Kiongozi wa Chama cha CHADEMA Zanzibar Dadi Kombo Maalim, akichangia mada katika Mkutano huo.
Mwandishi wa Jabir Idrisa akichangia mada zilizowasilishwa katika mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Habari Zanzibar.
Mwakilishi waJumuiya ya Wasioona Zanzibar Ahmeid Ali Omar, akichangia mada zilizowasilishwa na kuzitaka taasisi husika kuwatayarishia CD Watu wenye Ulemavu wa macho kupata habari kupitia njia hiyo ili waweze kuchangia mjadala wa Katiba.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, Amina Juma akichangia mada katika mkutano huo.
Bi Hasina Hamadi akichangia mada katika Mkutano huo.