Ndugu zangu,
Leo nilikwenda kwenye msiba wa binti wa binamu yangu pale Tosamaganga. Msiba ulikuwa na utata mkubwa. Wajomba wa mke wa baba wa marehemu wamegoma maiti kuzikwa kiu meni, Tosamaganga. Wametaka izikwe kijijini kwao Lupalama. Hoja yao? Mume wa mama wa marehemu ambaye pia ni marehemu , hakutoa mahari ya mke wake, ambaye pia ni marehemu- Kwamba 'Alifyagiza', kama inavyosemwa kimila. Kiumeni kaburi lilishachimbwa tangu jana. Na kikeni nako wameshachimba kaburi.
Ujumbe wetu ulifika kwa wajomba kijijini Lupalama kutafuta muafaka. Huko tulipokewa kama upepo. Yalikuwa ni ' mapokezi baridi' kupata kuyashuhudia. Ni baridi kushinda ile ya Mafinga. Hakuna aliyetuona wala kujaribu kutosogelea kuongea na sisi. Naam, Wajomba wa Kihehe walikasirika sana. Nahisi kulikuwa na ugomvi mwingine wa siku nyingi. Na kwenye kundi la Wajomba hakuonekana aliye tayari kutanguliza hekima na busara.
Niliziona dalili za kutokea kwa ugomvi mkubwa kama tungeendelea kubaki hapo. Inasemwa, chagua vita vyako. Vita vingine havina lazima ya kupiganwa. Vyaweza kuwa ni vita vya kiwendawazimu. Kwa nini mtu mzima ukubali kukiona kifaru chako kikitiwa kibiriti kwenye ' Vita vya Kiwendawazimu?
Na kulikuwa na hatari ya kupata hasara zaidi. Afrika msiba ni wa wote, hivyo basi, na maiti pia. Kwa nini watu wazima tugombanie maiti? Kisha turudi nyumbani kuzika wengine! Naam, ujumbe wetu ukaitafuta busara ya ' kutua mbanji'. Tukarudi nyumbani Tosamaganga na kuanza kufukia kaburi letu bila maiti. Wengi kwenye upande wetu wakawa ni wenye hasira sana. Kuna waliokuwa tayari kuuvunja undugu.
Nilipopata nafasi ya kushauri nikasema; kwa vile marehemu ameacha mtoto wa miaka mitano, basi, wenzetu wale watabaki kuwa ni ndugu zetu. Hasira za wajomba zikipungua, na za baadhi ya wa upande wetu, basi, watafutwe wazee wetu wenye hekima wa kwenda kufanya mazungumzo na wazee wenye hekima wa upande mwingine.
Na naamini, kuwa togwa litapikwa na tutakunywa kwa pamoja kutimiza mila na desturi zetu. Kwamba sote ni ndugu. Maggid, Iringa, 0788 111 765