Saturday, September 15, 2012

MH. PINDA AFUNGUA MRADI WA UFUGAJI NYUKI WILAYANI KWIMBA KATIKA ZIARA YAKE MKOA WA MWANZA



  
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akifungua mradi wa ufugaji nyuki katika kijiji cha Nkalalo wilayani kwimba akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza . Nyuma yake ni mkewe Mama Tunu na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Suleiman Mzee.
 
 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa wamevikwa mavazi ya kiongozi wa jadi wa Sungusungu katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Ngudu. 
 
 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Kwimba wakimsikiliza Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Ngudu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza.
 
Wasanii wa Kikundi cha Ng’wanadelema cha Ngudu wilayni Kwimba wakicheza ngoma ya Wayeye wakati Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alipowasalimia wnanchi katika kijiji cha Nkalalo wilayani Kwimba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).