Wednesday, September 19, 2012

MAONYESHO YA SOBER HOUSES RECOVERY ART EXHIBITION, ALLIANCE FRANCHISE, DAR OCTOBER 17-19 MWAKA HUU.




Drug Free Zanzibar (DFA) imeandaa maenyesho ya Sober House Recovery Art Exhibition. Katika maonyesho hayo vijana wanaoishi katika nyumba za kurekibishia tabia waathirika wa dawa za kulevya (Sober Houses) watapata fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika fani za uchoraji, ushonaji na uchongaji wa vitu mbalimbali. Pia wanajishughulisha mafunzo ya lugha za kiingereza na kifaransa, yoga, drama pamoja na shughuli  mbalimbali za uzalishaji mali .“Sober Houses” hizi zimesaidia mamia kwa mamia ya vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kuachana na matumizi ya dawa za kulevya wakiwemo watu maarufu katika fani mbalimbali. Lengo la haya yote ni kuwasaidia vijana ili warudi katika mstari na kurudi katika jamii zao stahiki.
Maonyesho haya yatafanyika katika ukumbi wa Alliance Franchise Upanga kuanzia tarehe 17 mpaka tarehe 19/10/2012, saa tatu asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni. Kiiingilio ni bure na wote mnakaribishwa kushiriki ili kuwasaidia na kuwatia moyo vijana wetu ambao wameamua kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kuwa mfano bora kwa vijana wenzao ambao bado wanajishughulisha na matumizi pamoja na biashara ya dawa hizi.
Kwa maelezo zaidi, kusaidia pamoja na ushauri unaweza kuwasiliana na ndg. Suleiman Mauly 0782 000426 au ndg. Alois Ngonyani 0713 334423/0686 334423