Thursday, September 27, 2012

KULIKONI JESHI LA POLISI NA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANGOSI.???


Jeshi la Polisi linatuhumiwa kutumia nguvu kuwadhibiti waandishi wa habari wasimpige picha askari Namba G.2573  Pacificus Cleophase Simon (23) anayeshitakiwa kwa tuhuma za kumuua Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Daudi Mwangosi.
Waandishi wa wamenusurika kupata kipigo kutoka kwa askari kanzu waliokuwepo mahakamani walipotaka kujaribu kuwapiga picha askari hao walipokuwa wakiendelea na harakati za kuwadhibiti wanahabari.
Askari Simon anadaiwa kumuua Mwangosi kwa kukusudia katika tukio lililotokea Septemba 2, mwaka huu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa kinyume na sheria namba 196 kifungu kidogo (i) sura ya 16, marejeo ya mwaka 2002.