Kiongozi wa upinzani wa Myanmar Bibi Aung San Suu Kyi (pichani) leo anatarajiwa kupokea medali ya dhahabu ya bunge la Marekani, ambayo ni heshima ya juu kabisa ya kiraia nchini humo.
Akiwa katika ziara ya siku 18 nchini Marekani, kiongozi huyo amesema anaunga mkono hatua zaidi za kulegeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo.
Bibi. Aung San Suu Kyi ameihimiza Myanmar kutopunguza kasi katika mchakato wa mageuzi ya kidemokrasi.