Friday, September 21, 2012

Kesi ya Lulu majaji wawabana mawakili





Utata wa umri wa Elizabeth Michael ‘LULU’ umechukua sura mpya baada ya jopo la majaji wa mahakama ya Rufani kuhoji waendesha mashitaka na mawakili wa Lulu kwanini wamelifikisha suala hilo mahakamani hapo badala ya kusubiri usikilizwaji wa awali.
Jopo la majaji hao, mwenyekiti Jaji January Msoffe, Bernard Luanda na Edward Rutakangwa walianza kuuhoji upande wa Jamhuri ni kwa sababu gani ameomba mahakama hiyo ifanye mapitio. Upande wa Jamhuri ukiongozwa na mwendesha mashitaka mwandamizi wa serikali Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro ulidai kuwa umeomba mapitio kwa sababu uamuzi uliotolewa na Jaji Dr Fauz Twaib. Bw. Nchimbi alikiri kwamba maombi ya utetezi hayakuwasilishwa mahakamani kihalali kwa mujibu wa sheria.
“Jaji Dr Twaib alikosea kutoa tafsiri ya kifungu 44 (1) cha sheria ya mahakimu alipaswa kutoa maelekezo kwa mahakama ya Kisutu kulingana na makosa aliyoyaona katika uamuzi wa hakimu mkazi Augustina Mmbando na siyo kuyasikiliza yeye mwenyewe…tumeamua kuomba mapitio ili yasikilizwe kwa haraka badala ya kukata rufaa,” alidai Nchimbi.