Wednesday, September 19, 2012

AJALI MBAYA MKOANI MBEYA: KAMBA YA KUFUNGIA NG'OMBE PAMOJA NA GOGO LA MTI VYATUMIKA KUFUNGIA USUKANI WA BASI LA ABIRIA.


 
 Sehemu ya chini ya usukani ukiwa umefungwa kwa kamba (ambayu hutumika kufungia ng'ombe) na mti kama uonavyo pichani,katika basi la abiria linalomilikiwa na Kampuni la Mwasha ambalo husafirisha abiria kutoka Sumbawanga/Mbeya na Mbeya/Sumbawanga. Hii imegunduliwa baada ya ajali iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Senjele,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya,baada ya basi hilo kupinduka ambapo zaidi ya abiria 50 walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Ifisi Wilaya ya Mbeya Vijijini.
 
 Baadhi ya mashuhuda wa ajali ya basi linalomilikiwa na Kampuni la Mwasha ambalo husafirisha abiria kutoka Sumbawanga/Mbeya na Mbeya/Sumbawanga. Hii imegunduliwa baada ya ajali iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Senjele,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
 
 Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa,akisubiri kupewa matibabu katika Hospitali ya Ifisi kufuatia ajali ya basi hilo lilolopinduka na kujeruhi abiria 50.
 
  Mmoja wa majeruhi akiwa mapumzikoni baada ya kupewa matibabu katika Hospitali ya Ifisi kufuatia ajali ya basi hilo lilolopinduka na kujeruhi abiria 50.
 
 Wauguzi wa Hospitali ya Ifisi wakikokota kitanda kilichobeba majeruhi wa ajali ya basi.
 
 Majeruhi akipatiwa matibabu.
 
Muuguzi Mkuu Sikitu Mbilinyi wa Hospitali ya Ifisi,akitoa taarifa ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali hiyo ya Ifisi,kufuatia ajali ya Kampuni la Mwasha ambalo husafirisha abiria kutoka Sumbawanga/Mbeya na Mbeya/Sumbawanga. Hii imegunduliwa baada ya ajali iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Senjele,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya,baada ya basi hilo kupinduka ambapo zaidi ya abiria 50 walijeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Ifisi Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Hata hivyo imedaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana na basi hilo kubeba mizigo mizito na kujaza abiria kupita kiasi na usukani wake kufungwa kamba ya katani na mti.
(Picha zote na Ezekiel Kamanga,Senjele)