Wednesday, August 08, 2012

Vodacom yasaidia watoto yatima Mkoani Mtwara.

Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mjini Mtwara,wakiwa katika hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya  Ramadhan Care & Share.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Mangochi Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami. akimkabidhi mfuko wenye unga wa kupikia ugali Bi.Chiku Mohamed aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia wapili toka kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Bw.Hassan Saleh, Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw.Ponsiano Nyami,akimkabidhi mtoto yatima ndoo ya mafuta ya kula Bi.Halima Juma, aliepokea kwa niaba ya watoto yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Shekh Mkuu wa Mkoa huo….Mkuu wa Vodacom kanda ya kusini Bw.Mac Minja,Ofisa Mkuu wa Mauzo na usambazaji Bw.Hassan Saleh na Mkuu wa Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule.

Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mtwara Bw Ponsiano Nyami,wapili toka kushoto pamoja na Shekh Mkuu wa Mkoa huo Bw.Nurdin Mangochi wakishuhudia Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Bw.Hassan Saleh akimkabidhi ndoo ya mafuta ya kula mtoto yatima Bi.Mwajuma Khamis aliepokea kwa niaba ya watoto wenzake yatima wa mkoa huo wakati wa hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share mjini humo inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Bw.Yessaya Mwakifulefule akimhudumia mtoto yatima Bi.Salha Haji uji mkoani Mtwara,aliefika kwenye hafla fupi ya kufuturisha na kutoa misaada mbalimbali,kupitia kampeni ya Ramadhan Care & Share  inaendeshwa na Vodacom Foundation,wakati wa mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Baadhi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Mtwara,wakifuturu wakati wa hafla fupi ya kufuturu na kukabidhiwa misaada mbalimbali iliyoandaliwa na
Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya  Ramadhan Care & Share mjini humo.

Vodacom yasaidia watoto yatima Mkoani Mtwara.

·        Ni kupitia kampeni ya Ramadhan Care and Share.

·        Ni katika mpango wa kuwathamini na kuwatambua Watoto waishio katika mazingira magumu.

·        Kampeni ya Mtwara ni ya pili baada ya kuzinduliwa  mkoani Tanga.

 

Mtwara,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki imetoa misaada mbalimbali na kuwafuturisha watoto yatima na wa madrasa wapatao 500 mkoani Mtwara kupitia kampeni yake ya Ramadhan Care and Share iliyo chini ya mfuko wa kusaidia jamii"Vodacom Foundation".

Misaada iliyotolewa kwa watoto hao ni pamoja na vifaa vya kujifunzia, vyakula,mafuta ya kula, mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid el fitr ikiwa ni katika kutimiza malengo ya mpango huo uliozinduliwa mapema wiki iliyopita mkoani Tanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Mkuu wa mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Bw.Hassan Saleh, mwezi mtukufu wa Ramadhan ni muhimu kwa waislamu wote nchini, sio tu kwa kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu, bali pia ni kipindi kinachowapa nafasi ya kuwafikiria na kuwajali wale wasio na uwezo ndani ya jamii yetu.

 "Kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tunaendesha kampeni hii katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua kuwa Waislamu walio wengi ni wateja wetu hivyo tumeona ni vyema kuwaenzi kwa kutoa kile tulichonacho katika sehemu ya mapato yetu ili nao wajisikie kuwa miongoni mwa jamii ya Watanzania," alisema Saleh.

Kampeni ya Ramadhan Care and Share imekuwa njia pekee ambayo Vodacom Foundation imekuwa ikiitumia katika kushughulikia maswala mbalimbali yanayowakumba watoto  yatima waishio katika mazingira magumu. Kupitia kampeni hii maisha ya makundi mbalimbali ya watoto yameweza kuboreshwa na kunufaika kutoka kwetu.

Kampeni hii ni moja kati ya kampeni nyingi ambazo yetu imeanzisha katika kipindi cha Ramadhan. Tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wateja wa malipo ya kabla wamewezeshwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno na kutumia intanet bila kikomo kwa shilingi 250 kwa siku.

Mwisho