Habari zilizoifikia Blog hii muda
mchache uliopita zinaeleza Kuwa wachungaji zaidi ya 2000 wameirejesha
Kamati Kuu Ya Kanisa Hilo Kuliongoza Tena Kanisa hilo Kongwe hapa
Tanzania.
Wachungaji asilimia 93 kati ya 2163 waliopiga kura Katika Uchaguzi Mkuu
Wa Tanzania Assemblies Of God Wamemrejesha Askofu Mkuu wa Kanisa hilo
Dr. Barnabas Mtokambali katika Nafasi yake ya Uaskofu. Dr. Mtokambali
amepata ushindi huo wa Kishindo baada ya kupendekezwa na wajumbe
kugombea tena nafasi hiyo.
Mchuano Mkubwa ulikuwa katika nafasi ya Makamu wa Askofu ambapo Dr.
Muhiche alichuana vikali na Bishop Kameta katika kinyang'anyiro hicho
Dr. Muhiche alifanikiwa kutetea kiti hicho kwa mara nyingine.
Pastor Ron Swai amechaguliwa tena kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God kwa mara nyingine.
Kwa maana hiyo Viongozi wote wa Kamati Kuu Wamefanikiwa Kutetea nafasi zao kwa miaka minne mingine.
Dr. Muhiche akiwashukuru Wajumbe wa Mkutano Mkuu baada ya Kumchagua kuwa Makamu wa Askofu kwa Mara nyingine.
Chaguzi za Maskafu wa Majimbo pamoja na Sehemu zinatarajiwa kuendelea
Siku Ya Kesho ambapo Mchuano Mkubwa unatazamiwa kuwepo kwenye Majimbo Ya
Dar-es-Salaam na Mikoa Kaskazini.