RAIS mpya wa Misri, Mohammed Morsi, amemteua waziri wa maji, Hisham Kandil, kama Waziri mkuu na kumuamuru aunde serikali.
Hadi kufikia sasa Bw Kandil hakuwa na sifa kubwa au umaarufu nchini Misri.
Na pia hatoki katika vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo Rais Morsi ni mwanachama wake.
Rais Morsi alikuwa ameahidi serikali itakayojumuisha raia wote wa Misri.
Kumekuwa na wasiwasi kuhusu mfumo atakaotumia bwana Musri kuteua baraza lake la mawaziri.
Jeshi la nchi lilimkabidhi rasmi mamlaka rais Mursi tarehe 30 mwezi Juni Juni, lakini bado linasalia kushukilia mamlaka makubwa tu juu ya taasisi kadhaa za nchi.
Tarehe kumi mwezi Julai, mahakama ya kikatiba ilitupilia uamuzi wa bwana Muris, kurejesha bunge la waakilishi ambalo lina wabunge wengi wa kiisilamu.
Uamuzi wake mwezi jana kufutilia mbali uchaguzi wa wabunge uliofanywa mapema mwaka huu kwa sababu ya makosa katika sheria, ilisababisha hali ya vuta nikuvute kisiasa.
Bwana Qandil alikuwa mwanachama wa serikali ya mpito iliyokuwa chini ya uongozi wa Kamal al-Ganzouri, aliyeteuliwa waziri mkuu mwaka jana.
"Uteuzi huu wa mtu ambaye hajulikani sana unajiri baada ya utafiti mkubwa kuhusu nani ateuliwe kuweza kukabiliana na hali ya sasa kisiasa."alisema msemaji wa rais Musri akiongeza kuwa bwana Qandil hana uhusiano wowote na chama chochote cha kisiasa kabla na baada ya mapinduzi ya kiraia dhidi ya utawala wa rais wa zamani Hosni Mubarak.
Bwana Qandil hajulikani sana nje ya Misri kwa sababu aliishi maisha yake pakubwa akifanya kazi katika sekta ya umma.
Akiwa na umri wa miaka 50, yeye ni waziri mkuu wa kwanza mwenye umri mdogo sana nchini Misri.
Bwana Mursi ni mwanchama wa chama cha Muslim Brotherhood, lakini ameahidi kuunda serikali ambayo itakuwa ya umoja kukiwa na uwakilishi wa wanwakena wakristo.