22 Julai, 2012 - Saa 14:31 GMT
Milio ya bunduki imesikika leo katika kambi ya jeshi karibu na uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.
Waziri wa ulinzi wa Madagascar aliliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP, kwamba kulitokea uasi jeshini, lakini haijulikani wanajeshi hao wanataka nini.
Waziri huyo wa Ulinzi Jenerali Lucien Rakotoarimasy hakusema wanajeshi wangapi walihusika.
Milio ya risasi imesita, lakini safari za ndege zimezuwiliwa.
Madagascar imekuwa ikipita kwenye misukosuko tangu mwaka wa 2009, wakati Marc Ravalomanana alipopinduliwa na jeshi.
Chanzo: BBC