Monday, July 02, 2012

TANGAZO KWA MADAKTARI WA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI


Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unawatangazia Madaktari wote ambao hawafiki kazini kuwa wanatakiwa kurudi kazini mara moja kwa kujiorodhesha majina yao kwa wakuu wao wa Idara.
Aidha, tangazo hili pia linawahusu Madaktari wote wanaokuja kazini lakini hawafanyi kazi, nao wajiorodheshe kwa wakuu wao wa Idara.
Wakuu wote wa Idara wanatakiwa kuwaorodhesha Madaktari wote watakaofika kazini kuanzia leo (2/Julai/2012) na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni, na taratibu zilizopo.
Zoezi hili litafungwa kesho tarehe 3 Julai 2012 saa tatu asubuhi.
Tangazo hili haliwahusu Madaktari walio katika Mafunzo kwa Vitendo (Interns).
Dr. Marina Njelekela,
Mkurugenzi Mtendaji
Saa 06:00 Mchana
Nakala: Wakurugenzi - Kwa usimamizi