Mchezaji wa Timu ya Azam,Khamis Mcha (22) akipimana ubavu na Shomari Kapombe wa Simba katika mchezo wa Mashindano ya Cecafa Kagame uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Azam ndio iliyoibuka kidedea kwa kuilambisha Simba Bao 3 -1.
Wachezaji wa Simba,Felix Sunzu (alieshika Mpira) na Haruna Moshi wakijiandaa kuanza mchezo baada ya kufungwa goli la kwanza.mpira umemalizika hivi punde uwanjani hapa na Azam wameweza ibuka washindi na kujikatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya kombe hilo la Kagame kwa ushindi wa Bao 3-1.
Kipa wa Azam,Deogratius Munisi akiondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.
Mshambuliaji wa Azam,Kipre Tchetche akiwazungusha Mabeki wa Simba katika mchezo wao uliopigwa jioni hii Uwanja wa Taifa Jijini Dar.Azam imeshinda bao 3-1.