Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Sylvia Gunza, akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Mishemishe za mkutano huo zikiendelea.
Mkurugenzi wa Ukuzaji Rasilimali wa mamlaka hiyo, Seif Mohamme, akijibu maswali ya wanahabari.
Mishemishe za mkutano huo zikiendelea.
Mkurugenzi wa Ukuzaji Rasilimali wa mamlaka hiyo, Seif Mohamme, akijibu maswali ya wanahabari.
MAMLAKA ya Elimu Tanzania leo imelipongeza Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na Kampuni ya Global Publishers Ltd, watoaji wa magazeti pendwa ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Gazeti hili na Risasi na mazageti ya michezo na burudani ya Championi.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa mamlaka hayo, Bi. Esther Bayo, wakati akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za mamlaka hiyo zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam alipotoa taarifa za uzinduzi wa mfuko wa kuchangia elimu unaotarajiwa kuzinduliwa Julai 14 mwaka huu.
Tamasha hilo lililokuwa na lengo la kuchangia kujenga sekondari za wanawake hapa nchini lilifanyika Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Bi. Boya amesema wa mfuko huo umepangwa kuzinduliwa kwenye mji mdogo wa Kibaigwa mkoani Morogoro ambapo kwa sasa una lengo la kukusanya kiasi sh bilioni mbili na laki tatu kwa ajili ya ujenzi wa sekondari nane za wasichana na mabweni yake 30.
Mkurugenzi huyo amesema kwa watakaochangia mfuko huo watapata hati maalum ya serikali na kupata punguzo la kodi katika shughuli zao
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL