Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa familia yake aliliambia NIPASHE jana kuwa, Dk. Ulimboka ameanza kutumia vifaa vya mazoezi na kufanya mazoezi mepesi mepesi.
Dk. Ulimboka aliyetekwa Juni 26, mwaka huu, alipigwa na kuumizwa mwili mzima, aling'olewa meno pamoja na kucha na watu wasiojulikana na kutupwa katika msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
SOURCE: NIPASHE