Monday, May 14, 2012

MAREHEMU RACHEL WA ‘MTANZANIA’ ALIVYOAGWA KANISANI UBUNGO

Mwili wa marehemu Rachel ukiwa kwenye jeneza.
Mmoja wa ndugu wa marehemu  akilia kwa uchungu.
Mama yake akiuaga mwili wa mwanaye.
Baba wa marehemu, Job Mwiligwa, akitoa heshima za mwisho
Dada wa marehemu akilia kwa uchungu.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kwenye gari kuelekea Goba.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (kushoto) akiwa na mbunge wa Wilaya ya Kinondoni, Mh. Idd Azan (kulia)
WATU mbalimbali leo wamekusanyika katika Kanisa la Anglicana, Ubungo, jijini Dar es Salaam, kuuaga mwili wa marehemu, Rachel Mwiligwa aliyekuwa mhariri wa gazeti la Mtanzania na aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Alhamisi wiki iliyopita  katika hospitali ya Mwananyamala.  Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mapafu.
Waliohudhuria ni pamoja na wabunge, wasanii wa muziki na waandishi wa habari ambapo mwili huo uliwasili kanisani  saa 5:30 kabla ya kupelekwa kuzikwa nyumbani kwao Goba jijini Dar.
                             HABARI/PICHA NA GLADNESS MALLYA, GPL